Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Qais Al-Khazali, Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq, siku ya Jumatano katika khutba ya Swala ya Idi ya Adh-ha mjini Baghdad, alisema kuwa; Muqawama haupaswi kuwekewa mipaka katika kazi za kijeshi pekee, bali ni mchakato unaoendelea kuelekea katika kulijenga taifa lenye nguvu na uwezo wa kufanya maamuzi ya kiutawala kwa uhuru.
Sheikh Al-Khazali alisema: Kazi ya kijeshi ya Muqawama ilihesabiwa kuwa kipaumbele cha kwanza katika kipindi ambacho serikali ya Iraq ilikuwa inakabiliwa na vitisho.
Alifafanua kwamba; fikra sahihi ya Muqawama inajidhihirisha katika kulijenga taifa lenye nguvu; taifa ambalo lina maamuzi yake ya kujitegemea, mamlaka yake na taasisi zake.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq alisisitiza kwamba: Muqawama wowote ambao hauna mradi kamili wa ujenzi, hatua kwa hatua utageuka kuwa mzigo kwa jamii.
Maoni yako